Sitanyamaza kamwe
Kwa sababu hiyo, Sitanyamaza kamwe Mpaka haki ipatikane Haki yako ipo Ninayaona yote
Sijakuita nikuache hapa
Sijakuita uishie hapa Nilikuita ili ufike mbali Naam Mbali kuliko hapa
Nalikujua wewe
Wakati ukiwa mdogo nalikujua, Wakati ungali kijana nalikutambua, Maisha yako yapo mikononi mwangu Ninazihesabu hatua zako zote Nimepanga kukupa wokovu Kwa maana mimi ndiye Mungu Niokoaye
Wewe ni Taa, Waangaze
Wewe ni Taa, Taa imulikayo Gizani Wenzio wako gizani, wewe ndio wa kuwaonyesha njia Mimi ni mwanga, Naam wewe upo na mimi Wamulike… Wajione Wamulikie… Wanifuate Kwa maana nawapenda wote.…
Sikia Mwanangu Sikiliza
Sikia MWanangu sikia… Kama vile baba mwema Ampendavyo mwanaye Ndivyo nami nakujali wewe Ninakupenda upeo