Mimi Ndimi Mimi
Mimi ni Nuru iangazayo Gizani Mimi ni Nuru ya njia yenu Mimi ni Njia ya wokovu wenu Mimi ni Wokovu wa Maisha yenu Mimi ni Ndiye kila kitu Naam… Huyo…
Mwanagu, Sikiliza sauti yangu nawe utanufaika
Mwanagu, Sikiliza sauti yangu nawe utanufaika… Tazama nimepnga mambo mengi mema kwako Naam… Yatakupata mema Mimi Mungu nimesema
Watie moyo walio wangu
Waambie watu wangu wajipe moyo Waambie wasihofu wala kufadhaika Kwa maana Mimi Naja kuwaokoa Sitawaacha, Kwa kuwa Mimi ni Mungu wao
Sijakuita nikuache hapa
Sijakuita uishie hapa Nilikuita ili ufike mbali Naam Mbali kuliko hapa
Nalikujua wewe
Wakati ukiwa mdogo nalikujua, Wakati ungali kijana nalikutambua, Maisha yako yapo mikononi mwangu Ninazihesabu hatua zako zote Nimepanga kukupa wokovu Kwa maana mimi ndiye Mungu Niokoaye
Jipe moyo, Mimi ni Mungu wako
Jipe moyo mwanagu kwa kuwa mimi ni Mungu wako. Hayo yote yatapita, Kama usiku uutanguliavyo mchana.