Mimi Ndimi Mimi
Mimi ni Nuru iangazayo Gizani Mimi ni Nuru ya njia yenu Mimi ni Njia ya wokovu wenu Mimi ni Wokovu wa Maisha yenu Mimi ni Ndiye kila kitu Naam… Huyo…
Mwanagu, Sikiliza sauti yangu nawe utanufaika
Mwanagu, Sikiliza sauti yangu nawe utanufaika… Tazama nimepnga mambo mengi mema kwako Naam… Yatakupata mema Mimi Mungu nimesema
Nalikujua wewe
Wakati ukiwa mdogo nalikujua, Wakati ungali kijana nalikutambua, Maisha yako yapo mikononi mwangu Ninazihesabu hatua zako zote Nimepanga kukupa wokovu Kwa maana mimi ndiye Mungu Niokoaye
Sikia Mwanangu Sikiliza
Sikia MWanangu sikia… Kama vile baba mwema Ampendavyo mwanaye Ndivyo nami nakujali wewe Ninakupenda upeo
Mimi ni Mungu nikupendaye
Nilikupenda na nitazidi kukupenda Kwa maana mimi ni Mungu wako Nikupendaye
Njoo Ujifunze Huruma na Upendo Wangu
Samehe nawe utasamehewa. Fadhili nawe utafadhiliwa. Hifadhi nawe utaifadhiwa. Naam, mimi ni Mungu nikupendaye na Kukuhurumia