• Sun. Mar 26th, 2023

Mungu.Me

Ujumbe wa Mungu Kwako

Tahadhari

  • Home
  • Kwa nini unaona haya juu yangu?

Kwa nini unaona haya juu yangu?

Kwa nini unanionea haya? Kwa nini unaona ugumu kunitaja? Je, mimi si ndiye niliyefanya haya yote?

Ni afadhali kunikubali kuliko kunikataa

Ni afadhali kunikubali mimi, kuliko kunikataa Kwa maana njia zangu ni njema Je, ni kawaida mtu kukataa kitu kizuri na kuchagua kibaya? La, Si kawaida.  Kama sio kawaida, wawezaje kunikataa?

Mimi Mungu huwezi kunificha kwa lolote

Mimi ndiye niliyekupa uwezo wa kufikiri na kuamua. Je, unazani unaweza kunificha kitu? Fahamu tuu kwamba ninajua yote.

Acha kuwaza na kunuia kufanya mabaya

Acha kuwaza na kunuia kufanya mambo mabaya, Kwa maana Unazuia Baraka na Rehema zako. Chunga nia na mawazo yako kwa kuwa ndiyo njia ya kuelekea kwenye matendo mabaya.