Fungua macho yako
Fungua Macho yako uone,
Kwa maana niko nawe lakini hunioni
Laiti ungetazama…
Ungeniona
Fungua Macho yako uone,
Kwa maana niko nawe lakini hunioni
Laiti ungetazama…
Ungeniona
Nalikuita, Ukaja.
Kwa nini unasita sasa?
Songa mbele…
Mimi ni Mungu wako Nikuongozaye
Kwa nini unanionea haya?
Kwa nini unaona ugumu kunitaja?
Je, mimi si ndiye niliyefanya haya yote?
Ni afadhali kunikubali mimi, kuliko kunikataa
Kwa maana njia zangu ni njema
Je, ni kawaida mtu kukataa kitu kizuri na kuchagua kibaya?
La, Si kawaida.
Kama sio kawaida, wawezaje kunikataa?
Rafiki…
Sikia sauti yangu na kupokea fundisho langu
Kwa maana huo ndio mwelekeo sahihi
Nuia kufanya Mambo mema mara zote, nawe utabarikiwa.
Kuwa na nia njema ni sawa na kutembea na Baraka zako.
Makusudio yako ndio Baraka zako
Kwa maana, ninaangalia nia za moyo wako, kwa kuwa huyo ndiyo wewe.
Mimi ni Mungu wako, ninayafahamu mawazo yako wakati wote.
Acha kuwaza na kunuia kufanya mambo mabaya, Kwa maana Unazuia Baraka na Rehema zako.
Matendo yako yanaongozwa na nia na mawazo yako.
Chunga nia na mawazo yako kwa kuwa ndiyo njia ya kuelekea kwenye matendo mabaya, kama ikiwa mbaya.