Mimi ndiye Mungu wako
Mimi ndiye Mungu wako
Mimi ni wa Mwanzo na Mwisho
Mimi ndiye wako sahihi wa kufuata
Nifuate unijue mimi
Mimi ndiye Mungu wako
Mimi ni wa Mwanzo na Mwisho
Mimi ndiye wako sahihi wa kufuata
Nifuate unijue mimi
Samehe nawe utasamehewa.
Fadhili nawe utafadhiliwa.
Hifadhi nawe utahifadhiwa.
Wawezaje kujua thamani ya Huruma na Upendo wangu usipowatendea wengine kwa Huruma na Upendo?
Naam, mimi ni Mungu nikupendaye na Kukuhurumia.
Wewe ni Taa, Taa imulikayo Gizani
Wenzio wako gizani, wewe ndio wa kuwaonyesha njia
Mimi ni mwanga, Naam wewe upo na mimi
Wamulike… Wajione
Wamulikie… Wanifuate
Kwa maana nawapenda wote.
Kwa maana nilivyokupenda wewe, nawapenda wao pia
Mimi ni Mungu wako, ninayafahamu mawazo yako wakati wote.
Acha kuwaza na kunuia kufanya mambo mabaya, Kwa maana Unazuia Baraka na Rehema zako.
Matendo yako yanaongozwa na nia na mawazo yako.
Chunga nia na mawazo yako kwa kuwa ndiyo njia ya kuelekea kwenye matendo mabaya, kama ikiwa mbaya.