Mwanagu Nisikilize
Rafiki…
Sikia sauti yangu na kupokea fundisho langu
Kwa maana huo ndio mwelekeo sahihi
Rafiki…
Sikia sauti yangu na kupokea fundisho langu
Kwa maana huo ndio mwelekeo sahihi
Mimi ndiye Mungu wako
Mimi ni wa Mwanzo na Mwisho
Mimi ndiye wako sahihi wa kufuata
Nifuate unijue mimi
Fungua Macho yako uone,
Kwa maana niko nawe lakini hunioni
Laiti ungetazama…
Ungeniona
Kwa nini unanionea haya?
Kwa nini unaona ugumu kunitaja?
Je, mimi si ndiye niliyefanya haya yote?
Mimi ni Nuru iangazayo Gizani
Mimi ni Nuru ya njia yenu
Mimi ni Njia ya wokovu wenu
Mimi ni Wokovu wa Maisha yenu
Mimi ni Ndiye kila kitu
Naam… Huyo Ndiyo Mungu Wenu
Mwanagu, Sikiliza sauti yangu nawe utanufaika…
Tazama nimepnga mambo mengi mema kwako
Naam… Yatakupata mema
Mimi Mungu nimesema
Nalikuita, Ukaja.
Kwa nini unasita sasa?
Songa mbele…
Mimi ni Mungu wako Nikuongozaye