Jipe moyo mwanagu kwa kuwa mimi ni Mungu wako. Hayo yote yatapita, Kama usiku uutanguliavyo mchana.
Mwanagu, acha dhambi zako na unirudie mimi. Ninayafahamu mapungufu yako na madhaifu yako. Tubu kwa moyo wako wote nami nitafanya njia
Kama ilivyo kwa mzazi anavyotamani kumfanyia mwanae mambo mazuri, Ndivyo nami ninavyokuwazia wewe Naam, ninakuwazia mema na ninalenga kukutendea jambo jema
Acha kuwaza na kunuia kufanya mambo mabaya, Kwa maana Unazuia Baraka na Rehema zako. Chunga nia na mawazo yako kwa kuwa ndiyo njia ya kuelekea kwenye matendo mabaya.
Nuia kufanya Mambo mema mara zote, nawe utabarikiwa. Kwa maana, ninaangalia nia za moyo wako, kwa kuwa huyo ndiyo wewe.