Mimi Ndimi Mimi
Mimi ni Nuru iangazayo Gizani Mimi ni Nuru ya njia yenu Mimi ni Njia ya wokovu wenu Mimi ni Wokovu wa Maisha yenu Mimi ni Ndiye kila kitu Naam… Huyo…
Mimi Mungu huwezi kunificha kwa lolote
Mimi ndiye niliyekupa uwezo wa kufikiri na kuamua. Je, unazani unaweza kunificha kitu? Fahamu tuu kwamba ninajua yote.
Usitishwe na chochote, Mimi nipo
Furahia shangilia wewe uliye wangu. Uambie Moyo wako upo salama kwa Mungu wako. Kwa maana, Mungu wako ni Mkuu kati ya hao wote