Jipe moyo, Mimi ni Mungu wako
Jipe moyo mwanagu kwa kuwa mimi ni Mungu wako
Hayo yote yatapita, Kama usiku uutanguliavyo mchana
Pambazuko laja na Baraka zako
Naam, Mimi ni Mungu wako
Jipe moyo mwanagu kwa kuwa mimi ni Mungu wako
Hayo yote yatapita, Kama usiku uutanguliavyo mchana
Pambazuko laja na Baraka zako
Naam, Mimi ni Mungu wako
Kwa nini unanionea haya?
Kwa nini unaona ugumu kunitaja?
Je, mimi si ndiye niliyefanya haya yote?
Rafiki…
Sikia sauti yangu na kupokea fundisho langu
Kwa maana huo ndio mwelekeo sahihi
Nuia kufanya Mambo mema mara zote, nawe utabarikiwa.
Kuwa na nia njema ni sawa na kutembea na Baraka zako.
Makusudio yako ndio Baraka zako
Kwa maana, ninaangalia nia za moyo wako, kwa kuwa huyo ndiyo wewe.
Nalikuita, Ukaja.
Kwa nini unasita sasa?
Songa mbele…
Mimi ni Mungu wako Nikuongozaye
Samehe nawe utasamehewa.
Fadhili nawe utafadhiliwa.
Hifadhi nawe utahifadhiwa.
Wawezaje kujua thamani ya Huruma na Upendo wangu usipowatendea wengine kwa Huruma na Upendo?
Naam, mimi ni Mungu nikupendaye na Kukuhurumia.
Ni afadhali kunikubali mimi, kuliko kunikataa
Kwa maana njia zangu ni njema
Je, ni kawaida mtu kukataa kitu kizuri na kuchagua kibaya?
La, Si kawaida.
Kama sio kawaida, wawezaje kunikataa?