Fungua macho yako
Fungua Macho yako uone, Kwa maana niko nawe lakini hunioni Laiti ungetazama… Ungeniona
Kwa nini unaona haya juu yangu?
Kwa nini unanionea haya? Kwa nini unaona ugumu kunitaja? Je, mimi si ndiye niliyefanya haya yote?
Mimi Ndimi Mimi
Mimi ni Nuru iangazayo Gizani Mimi ni Nuru ya njia yenu Mimi ni Njia ya wokovu wenu Mimi ni Wokovu wa Maisha yenu Mimi ni Ndiye kila kitu Naam… Huyo…
Wewe ni Taa, Waangaze
Wewe ni Taa, Taa imulikayo Gizani Wenzio wako gizani, wewe ndio wa kuwaonyesha njia Mimi ni mwanga, Naam wewe upo na mimi Wamulike… Wajione Wamulikie… Wanifuate Kwa maana nawapenda wote.…
Mimi ni Mungu nikupendaye
Nilikupenda na nitazidi kukupenda Kwa maana mimi ni Mungu wako Nikupendaye
Mimi ni Mungu Nikuwaziaye Mema
Kama ilivyo kwa mzazi anavyotamani kumfanyia mwanae mambo mazuri, Ndivyo nami ninavyokuwazia wewe Naam, ninakuwazia mema na ninalenga kukutendea jambo jema