Nalikuita, Ukaja. Kwa nini unasita sasa? Songa mbele… Mimi ni Mungu wako Nikuongozaye
Waambie watu wangu wajipe moyo Waambie wasihofu wala kufadhaika Kwa maana Mimi Naja kuwaokoa Sitawaacha, Kwa kuwa Mimi ni Mungu wao
Ni afadhali kunikubali mimi, kuliko kunikataa Kwa maana njia zangu ni njema Je, ni kawaida mtu kukataa kitu kizuri na kuchagua kibaya? La, Si kawaida. Kama sio kawaida, wawezaje kunikataa?
Kwa sababu hiyo, Sitanyamaza kamwe Mpaka haki ipatikane Haki yako ipo Ninayaona yote
Sijakuita uishie hapa Nilikuita ili ufike mbali Naam Mbali kuliko hapa
Wakati ukiwa mdogo nalikujua, Wakati ungali kijana nalikutambua, Maisha yako yapo mikononi mwangu Ninazihesabu hatua zako zote Nimepanga kukupa wokovu Kwa maana mimi ndiye Mungu Niokoaye