Twende tusonge mbele
Nalikuita, Ukaja.
Kwa nini unasita sasa?
Songa mbele…
Mimi ni Mungu wako Nikuongozaye
Nalikuita, Ukaja.
Kwa nini unasita sasa?
Songa mbele…
Mimi ni Mungu wako Nikuongozaye
Mimi ndiye Mungu niliyekuumba
Mimi ndiye niliyekupa uwezo wa kufikiri na kuamua
Je, unazani unaweza kunificha kitu?
Kwa nini unasema neno jema na kunuia neno baya?
Fahamu tuu kwamba ninajua yote.
Kwa nini unanionea haya?
Kwa nini unaona ugumu kunitaja?
Je, mimi si ndiye niliyefanya haya yote?
Waambie watu wangu wajipe moyo
Waambie wasihofu wala kufadhaika
Kwa maana Mimi Naja kuwaokoa
Sitawaacha, Kwa kuwa Mimi ni Mungu wao
Jipe moyo mwanagu kwa kuwa mimi ni Mungu wako
Hayo yote yatapita, Kama usiku uutanguliavyo mchana
Pambazuko laja na Baraka zako
Naam, Mimi ni Mungu wako
Mimi ni Mungu wako, ninayafahamu mawazo yako wakati wote.
Acha kuwaza na kunuia kufanya mambo mabaya, Kwa maana Unazuia Baraka na Rehema zako.
Matendo yako yanaongozwa na nia na mawazo yako.
Chunga nia na mawazo yako kwa kuwa ndiyo njia ya kuelekea kwenye matendo mabaya, kama ikiwa mbaya.
Rafiki…
Sikia sauti yangu na kupokea fundisho langu
Kwa maana huo ndio mwelekeo sahihi